Friday, July 25, 2025

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

Na, Mudishatv blog

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, leo Julai 24, 2025, amefanya kikao na wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa ajili ya kuimarisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa mazao.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu huu umeboreshwa kwa kuzingatia changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.

Ameeleza kuwa mojawapo ya maboresho makubwa ni kuongezeka kwa vituo vya ukusanyaji kutoka viwili hadi nane, jambo ambalo litaongeza ufanisi na kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Katika kikao hicho, wadau kwa pamoja wamekubaliana kuwa uzalendo ni msingi wa maendeleo ya Hanang, wakisisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kutekeleza mpango huo.

Thursday, May 22, 2025

WANANCHI NJOMBE WAFURAHIA HUDUMA YA KUUNGANISHIWA UMEME KUPITIA REA




WANANCHI NJOMBE WAFURAHIA HUDUMA YA KUUNGANISHIWA UMEME KUPITIA REA

Wananchi wa vitongoji na vijiji mbalimbali vya  Mkoa wa Njombe wameonesha kufurahia huduma za usambazaji na uunganishaji umeme vijijini kupitia REA.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa umma kuhusu miradi ya kusambaza umeme vijijini, wananchi wa mkoa wa Njombe wamesema wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea huduma ya umeme kwa gharama nafuu ya Shilingi 27,000/- tu.



Pia, wananchi hao wamefurahia huduma ya kifaa cha Umeme-tayari (Ready-board) ambacho kinamuwezesha mwanachi  kuunganishiwa umeme bila ya kufanya wiring katika nyumba. Aidha, wameipongeza Serikali kupitia REA kwa huduma hiyo kwa kuwa inawapunguzia gharama za wiring. 



Mkazi wa Kijiji cha Ihanga. Christina Mlowe,  amesema " Mimi mjane mmeniwekea huu umeme wa kupunguza gharama za wiring, sikutegemea haya, nitautumia kwa watoto kusomea na kuchaji simu, nashukuru sana"



Kwa upande wake, Fabian Ngailo mkazi wa kijiji cha Makewe amesema, "baada ya kupata umeme huu, najipanga kujenga nyumba kubwa na kuweka umeme pamoja na mashine ya kusaga". Aidha, wameeleza kuwa kwa sasa hawatalala giza, na wataweza kununua TV na radio kwa kuwa sasa wana umeme kwenye nyumba zao.


Friday, March 21, 2025

WENYEVITI 3 WA KIJIJI NA VITONGOJI KITETO WATIWA HATIAN KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

 

WENYEKITI 3 WA KIJIJI NA VITONGOJI WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

NA MWANDISHI WETU, KITETO.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kiteto, imewatia hatiani viongozi watatu wa Kijiji cha Engusero, Robert Mtyambui (mwenyekiti wa kitongoji), Mochiwe Mkinya ( mwenyekiti wa kitongoji cha Engusero) na Bw. Jarome Mkunda (mwenyekiti wa kitongoji cha Mabululu) 

Viongozi hao wanatuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 28(1) na 31 vya Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya 2022.

Hukumu hiyo imetolewa Machi 21, 2025 na Hakimu mkaxi wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto Boniface Lihameike katika shauri  la Uhujumu uchumi Na. 03/2025. 

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda makosa kuuza maeneo ya Kijiji bila kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa kijiji cha Engusero kinyume na kifungu cha 8(5) cha sheria ya ardhi ya vijiji. 

Washtakiwa hao walikiri kutenda makosa hayo na Mahakama imewatia hatiani na kuamuru walipe faini Tshs. 50,000/= kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na kurejesha kiasi cha shilingi 2,660,000 ambazo zimerejeshwa kwenye akaunti ya TAKUKURU Mkoa wa Manyara. 

Hata hivyo watuhumiwa hao na viongozi wa Serikali walilipa faini hiyo kwa pamoja na kurejea nyumbani kwao.


Mwisho

Tuesday, February 11, 2025

HUJMA BWAWA LA NYERERE,KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI MAGAZETI FEB 12.2025

 Karibu Mudisha tv, tupitie vichwa vya magazeti kwa pamoja, vilivyoandakwa kwenye magazeti ya Tanzania leo Feb 12.2025

















Friday, January 31, 2025

Wednesday, January 29, 2025

WASIRA AISHUKIA CHADEMA, KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI MAGAZETI YA LEO JAN 30.2025

 Karibu Mudisha tv, tupitie vichwa vya magazeti kwa pamoja, vilivyoandakwa kwenye magazeti ya Tanzania leo Jan30.2025











Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post