DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI
Na, Mudishatv blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, leo Julai 24, 2025, amefanya kikao na wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa ajili ya kuimarisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa mazao.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu huu umeboreshwa kwa kuzingatia changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.
Ameeleza kuwa mojawapo ya maboresho makubwa ni kuongezeka kwa vituo vya ukusanyaji kutoka viwili hadi nane, jambo ambalo litaongeza ufanisi na kuwafikia wakulima wengi zaidi.
Katika kikao hicho, wadau kwa pamoja wamekubaliana kuwa uzalendo ni msingi wa maendeleo ya Hanang, wakisisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kutekeleza mpango huo.



