Friday, March 21, 2025

WENYEVITI 3 WA KIJIJI NA VITONGOJI KITETO WATIWA HATIAN KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

 

WENYEKITI 3 WA KIJIJI NA VITONGOJI WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

NA MWANDISHI WETU, KITETO.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kiteto, imewatia hatiani viongozi watatu wa Kijiji cha Engusero, Robert Mtyambui (mwenyekiti wa kitongoji), Mochiwe Mkinya ( mwenyekiti wa kitongoji cha Engusero) na Bw. Jarome Mkunda (mwenyekiti wa kitongoji cha Mabululu) 

Viongozi hao wanatuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 28(1) na 31 vya Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya 2022.

Hukumu hiyo imetolewa Machi 21, 2025 na Hakimu mkaxi wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto Boniface Lihameike katika shauri  la Uhujumu uchumi Na. 03/2025. 

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda makosa kuuza maeneo ya Kijiji bila kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa kijiji cha Engusero kinyume na kifungu cha 8(5) cha sheria ya ardhi ya vijiji. 

Washtakiwa hao walikiri kutenda makosa hayo na Mahakama imewatia hatiani na kuamuru walipe faini Tshs. 50,000/= kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na kurejesha kiasi cha shilingi 2,660,000 ambazo zimerejeshwa kwenye akaunti ya TAKUKURU Mkoa wa Manyara. 

Hata hivyo watuhumiwa hao na viongozi wa Serikali walilipa faini hiyo kwa pamoja na kurejea nyumbani kwao.


Mwisho

Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post