Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Waziri Athumani Sango, maarufu Waziri Fonyoo miaka (39) mkazi wa Sunya amedaiwa kukutwa porini ameuawa na watu wasiojulikana akiwa na majeraha ya kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake
Imeelezwa mtu huyo alikuwa ni mchungaji wa mifugo, tukio hilo limetokea leo Dec 10.2024, na kwamba mmiliki wa mifugo hiyo yeye anajulikana kwa jina la Hassani Ngor Kinyemba (22)
Imeelezwa mpaka sasa wananchi wanaendelea kutafuta mifugo hiyo porini ambapo chanzo cha habari hizi kinasema watuhumiwa wametoweka na mifugo hiyo na wanahisi wao ndio wamefanya tukio hilo.
Chanzo cha habari hizi kinasema mwili wa mmarehemu umechukuliwa na kuhifadhiwa Kituo cha afya Sunya huku wananchi hao wakiomba Jeshi la Polisi kuungana pamoja kuwasaka wahalifu hao.
Mudisha tv tunaendelea kumtafuta kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara kuhusu tukio hili na mara baada ya kumpata tutakuja na habari hizi zaidi.


No comments:
Post a Comment