Monday, November 18, 2024

MGOGORO WA MPAKA WA KITETO NA KILINDI WANUKIA..

(Picha ya kuchomwa gari aina ya Noah ambayo ni chanzo cha migogoro hiyo)


 Na Mohamed CHUMVI

Mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kiteto eneo la Lembapuli na Wilaya ya Kilindi eneo la mafisa unanukia.

Wananchi wanaoishi mpakani mwa wilaya hizo wamejawa na hofu baada ya kudaiwa kuibuka baadhi ya wananchi kutembea na silaha huku kukiwa na vitishi

Wananchi hao wanagombea ardhi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ambapo mpaka unatajwa kuwa chanzo cha mgogoro huo

"Wananchi wa mafisa wanatembea na silaha (bunduki) sisi Kiteto tulishapokonywa silaha zetu siku nyingi hivyo tunashindwa kujil8nda" kimesema chanzo cha habari hizi

"Tunatii sheria Kiteto lakini wenzetu hawatii na wanekuwa tishio sasa wanavamia maeneo ya Kiteto Lembapuli wakitokea mafisa kwa ajili ya kulima"amesema

Kwa upande wa wananchi wa mafisa ambao ni wakulima wamesema wananchi wa Kiteto jamii ya maasai wanawakataza kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo yao

"Hawa wenzetu wa Kiteto maasai eneo la Lembapuli ni jeuri sana wao wanadai maeneo tunayolima miaka yote kuwa ni yao na wanatukataza wanatupiga na silaha za jadi" amesema mmoja wa wananchi Kilindi

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post