Na Mohamed Chumvi
Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amesikia kilio cha mtoto HUSSEIN(16) mwenye tatizo la saratani ya kichwa na kuagiza afikishwe hosp ya Benjamini Mkapa kwa matibabu
Awali mtoto huyo alirejeshwa nyumbani baada ya wazazi wake kukosa fedha za matibabu hali iliyotishia ustawi wa maisha yake
Mtoto HUSSEIN ambaye wazazi wake ni wakazi wa Babati vijijini mkoani Manyara, alipata tatizo la saratani ya Kichwa miaka michache iliyopita na kutishia maisha yake.
Akizungumza na Mudisha tv Dr. Humber BMH wa hospitali ya Benjamini Mkapa alisema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imesikia kilio hicho cha mtoto huyo akiomba msaada wa matibabu baada ya Mudisha tv kuripoti.
"Baada ya Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kusikia kilio cha mtoto huyu akiomba msaada wa matibabu nimeagizwa kufuatilia na sasa tumempokea saa saba usiku kuamkia Dec 26.2024 Hospitali ya Benjamin Mkapa baada ya Serikali ya Mkoa wa Manyara kumsafirisha na sasa anaendelea na matibabu yake"amesema Dr Humber.


No comments:
Post a Comment