Friday, December 20, 2024

RAIS SAMIA AWAPA FARAJA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO HANANG

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) , leo Disemba 20, 2024, Amezindua na kukabidhi nyumba 109 katika kijiji cha Waret kwa waathirika wa maporomoko ya mawe na matope yaliyotokea Wilayani Hanan'g  Mkoani  Manyara mwaka jana tarehe 3 Disemba,2023.

Akikabidhi Nyumba hizo, hati, funguo na majiko ya gesi kwa wana kaya 20 kwa niaba ya kaya 109  za wahanga hao, ambapo Mkuu wa Mkoa atarudi kukabidhi hati zilizo baki kwa kaya 89, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa serikali inatambua mchango  wa watu wote walioshiriki katika kuokoa na kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo Chakula,mavazi, na malazi.

Pamoja na kutoa shukrani hizo kwa wadau,wa maendeleo wakiwemo Tanzania Red Cross Waziri mkuu ameuelekeza uongozi wa Mkoa na Wilaya  kusimamia uendelezaji wa kitongoji hicho cha waret na kusimamia ukamilishwaji wa miundombinu inayoendelea kujengwa hapo ikiwemo Shule, Zahanati na Soko.

Aidha, kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Serikali   ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea makazi Mapya waathirika hao. Ameahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post