WAFUGAJI WALIOUZA NYANDA ZA MALISHO KWA AJILI YA KILIMO, WAREJESHE FEDHA HIZO KWA WENYEWE..
Na Mohamed CHUMVI
IMEELEZWA kuwa wafugaji waliouza ardhi ili wajipatie fedha kwa ajili ya kuongeza mifugo yao, warejeshe fedha hizo kwa wahusika ambao ni wakulima kwani hawatoruhusiwa kulima nyanda za malisho
Mfugaji huna mamlaka ya kuuza ardhi ya malisho, kwa waliouza ardhi na kupata fedha kza uongeza mifugo yao, waiuze mifugo hiyo na kurejesha fedha kwa wakulima hao ambao lengo lao ni kufanya shughuli za kilimi
Mwenyekiti wa Nyanda za malisho Kiteto, Meshack Saskari akizungumza na Mudisha Tv amesema baadhi ya wafugaji wamekuwa wasumbufu kwa Serikali
"Fedha ulizopata wewe mfugaji kwa kuuza ardhi isivyo halali rejesha kwa mhusika kwani huna mamlaka ya kuuza ardhi hiyo na hii ndiyo inayochangia migogoro ya ardhi Kiteto kila kukicha"amesema Meshack
Nawataka waliouza ardhi na kupata fedha warejeshe fedha hizo haraka kwa mkulima ili naye atafute maeneo mbadala ya kilimo cha msimu huu na hii itapunguza sana mgogoro baina ya wakulima na wafugaji
Meshack ametoa wito kwa viongozi hao wa Serikali kuwachukulia hatua wenye tabia za kuuza ardhi na kwa sasa migogoro hii inaendelea kuhatarisha maisha ya watu amesisitiza Meshaki
Mwisho

No comments:
Post a Comment