Sunday, December 22, 2024

RC SENDIGA ATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

 Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, Disemba 22, 2024 amegawa hati za nyumba, funguo za nyumba, majiko ya gesi pamoja na miti ya matunda kwa kaya 89 za walioathirika wa maporomoko ya tope ya mlima Hanang ambao hawakupatiwa hati wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo.

RC Sendiga, amefanya zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Kassim Majaliwa  Majaliwa (Mb) , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Disemba 20, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Makazi hayo Mapya ya waathirika wa maporomoko ya matope.

Akizungumza na wanufaika wa nyumba hizo RC  Sendiga amewaasa kuishi kwa upendo na amani, wanapaswa kuzitunza nyumba hizo ikiwemo kuzingatia usafi na kuboresha mazingira yanayowazunguka.

Baadhi ya wanufaika wa nyumba hizo wametoa shukrani zao kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa wamezifurahia huku wakiahidi kuzitunza na kutunza mazingira hayo.



Saturday, December 21, 2024

KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI SOTE MAGAZETI YA TANZANIA DEC 22.2024

Karibu Mudisha tv, tupitie vichwa vya magazeti kwa pamoja, vilivyoandakwa kwenye magazeti ya Tanzania leo Dec.22. 2024












Friday, December 20, 2024

RAIS SAMIA AWAPA FARAJA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO HANANG

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) , leo Disemba 20, 2024, Amezindua na kukabidhi nyumba 109 katika kijiji cha Waret kwa waathirika wa maporomoko ya mawe na matope yaliyotokea Wilayani Hanan'g  Mkoani  Manyara mwaka jana tarehe 3 Disemba,2023.

Akikabidhi Nyumba hizo, hati, funguo na majiko ya gesi kwa wana kaya 20 kwa niaba ya kaya 109  za wahanga hao, ambapo Mkuu wa Mkoa atarudi kukabidhi hati zilizo baki kwa kaya 89, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa serikali inatambua mchango  wa watu wote walioshiriki katika kuokoa na kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo Chakula,mavazi, na malazi.

Pamoja na kutoa shukrani hizo kwa wadau,wa maendeleo wakiwemo Tanzania Red Cross Waziri mkuu ameuelekeza uongozi wa Mkoa na Wilaya  kusimamia uendelezaji wa kitongoji hicho cha waret na kusimamia ukamilishwaji wa miundombinu inayoendelea kujengwa hapo ikiwemo Shule, Zahanati na Soko.

Aidha, kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Serikali   ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea makazi Mapya waathirika hao. Ameahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu.

KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI VICHWA VYA HABARI DEC 21.2024

 Karibu Mudisha tv, tupitie kwa pamoja vichwa vya habari, vilivyoandaliwa kwenye magazeti ya Tanzania siku ya leo Dec 21.2024.












Wednesday, December 18, 2024

MGOGORO WA MPAKA KATI YA KITETO NA KILIINDI WANUKIA TENA...HOFU YATANDA..

 

(Picha ya kuchomwa gari ambayo ilikuwa chanzo cha mgogoro huo)

 Na Mohamed CHUMVI

Mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kiteto eneo la Lembapuli na Wilaya ya Kilindi eneo la mafisa unanukia.

Wananchi wanaoishi mpakani mwa wilaya hizo wamejawa na hofu baada ya kudaiwa kuibuka baadhi ya wananchi kutembea na silaha huku kukiwa na vitishi

Wananchi hao wanagombea ardhi hiyo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ambapo mpaka unatajwa kuwa chanzo cha mgogoro huo

"Wananchi wa mafisa wanatembea na silaha (bunduki) sisi Kiteto tulishapokonywa silaha zetu siku nyingi hivyo tunashindwa kujil8nda" kimesema chanzo cha habari hizi

"Tunatii sheria Kiteto lakini wenzetu hawatii na wanekuwa tishio sasa wanavamia maeneo ya Kiteto Lembapuli wakitokea mafisa kwa ajili ya kulima"amesema

Kwa upande wa wananchi wa Kijiji cha Mafisa Kilindi ambao ni wakulima wao wamesema baadhi ya wananchi wa Kiteto eneo la Lembapuli jamii ya maasai wanawakataza kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo yao

"Hawa wenzetu wa Kiteto maasai eneo la Lembapuli ni jeuri sana wao wanadai maeneo tunayolima miaka yote kuwa ni yao na wanatukataza wanatupiga na silaha za jadi" amesema mmoja wa wananchi Kilindi

Kwa hali iliyofikia kinachotakiwa ni kikao cha ujirani mwema kati ya pande hizo kutafsiri maamuzi na maelekezo mbalimbali ya Serikali ili wananchi hao waweze kuelewa na kufuata sheria

Mwisho

KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI VICHWA VYA MAGAZETI YA TANZANIA DEC 19.2024

 Karibu Mudisha tv, tupitie kwa pamoja vichwa vya habari, vilivyoandaliwa kwenye magazeti ya Tanzania siku ya leo Dec 19.2024.
















Sunday, December 15, 2024

KARIBU MUDISHA TV TUPERUZI VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA TANZANIA LEO DEC 16.2024

Karibu Mudisha tv, tupitie kwa pamoja vichwa vya habari, vilivyoandaliwa kwenye magazeti ya Tanzania siku ya leo Dec 16.2024.













 

Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post