Na, Mohamed CHUMVI, Kiteto
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Emmanuel Mwema, amewatahadharisha wananchi wilayani humo, kuepuka madhara yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa na kusababisha madhara yakiwemo baadhi ya watu kupoteza maisha pamoja na mali zao.
DC Mwema amewataka wananchi hao kuwa mkini na pia wachukue tahadhari ya mvua hizo kwani pamoja na Serikali kuweka mazingira mazuri na bora kama vile upatikanaji wa huduma za jamii bado jamii inalojukumu la kufanya
"Unapofika wakati wa msimu wa mvua wananchi chukueni tahadhari katika makazi yanu na katika shughuli zenu za kawaida..Mimi tayari nimeshaunda timu inayozunguka wilaya yote ya Kiteto kuona maeneo hatarishi"amesema Mwema
Amesema kuna timu ya maafa inafanya kazi kubwa ya kuona makazi ya watu na endapo mvua kubwa zitanyesha kuathiri mashamba ya watu, mifuko nakadhalika, nimetoa melekezo kwa taasisi mfano tanesco kuona namna gani watakavyoboresha kazi zao hali kadhalika Tarura na Ruwasa.
Nimetoa maelekezo pia kwa watendaji wa vijiji na wenyeviti kwenye maeneo yao mvua zinaponyesha wawe wanatoa taarifa kwa wakati..kama kuna maeneo mengine ni tishio, madimbwi, makorongo waseme ili tutoe tahadhari kwa wananchi
Tahadhari nyingine ni kwa watoto na wanafunzi hawa wakati mwingine mvua zinaponyesha wasisogelee maji ambayo yanamadhara na wazazi nao waendelea kuwa karibu nao wanapokuwa nyumbani
Katika hatua hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka viongozi wa kada mbalimbali wilayani humo kutimiza wajibu wao akisema pasiwe na kiongozi ndani ya jamii ambaye hafanyi kazi huku wananchi wakihitahi huduma yake bila mafanikio/
No comments:
Post a Comment