Friday, December 6, 2024

DKT. BITEKO; NISHATI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU...






Na Said Njuki, Arusha

WADAU wa maendeleo wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) zimetakiwa kujikita teknolojia ili kurahisisha utekelezaji za mipango ya matumizi ya Nishati Bora.

Aidha, wadau hao wamehimizwa kuweka mikakati imara ya kuchangia uwekezaji katika Nishati Bora na Safi kwa lengo la kusaidia ongezeko la upatikanaji wa Nishati hiyo ili kupunguza matumizi ya Nishati duni kwenye maeneo yao.

Rai hiyo, ilitolewa jana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko jijini Arusha, wakati akifungua mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati.



"Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na zile za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) zina wajibu mkubwa wa kuimarisha teknolojia na kuwa na mipango thabiti juu ya utafiti ili kuwa na uhakika wa Nishati bora, hivyo kuweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu lakini pia kukuza uchumi endelevu katika maeneo husika".Alisema Dkt. Biteko. 

Alisema zipo changamoto kadhiia wa kadha zinazoikabili b hiyo, lakini wanapambana nazo na hapana shaka matumizi ya Nishati Bora hkupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za kibiashara kutoka juu kabisa hadi ngazi ya Kaya.

"Biashara zinaweza kuongezeka na kuleta ushindani kwa kuzifanya ziwe thabiti zaidi katika masomo ya ndani ya Kimataifa yanayobadilika mara kwa mara, hivyo kupunguza utegemezi wa Nishati kutoka nje ikiwa tutaboresha matumizi ya Nishati yetu".alisisituza Dkt. Biteko.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba aliitaka jamii kutumia Nishati kwa uangalifu kwani Nishati hiyo ni rasilimali ya Taifa na haitakiwa kuchezewa hivyo ni wajibu kuitunza kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.

"Punguza matumizi ya kiyoyozi kwa kufungua madirisha pale inapobidi, tumia mashine ya kufulia nguo wakati matumizi ya umeme yapo chini ili kupunguza mzigo kwenye gridi ya taifa...tumia maji kwa uangalifu kwa kufunga vifaa vinavyotunza maji hivyo kuokoa bili za umeme na maji zisiwe kubwa".alisisituza Mhandisi Mramba.


Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Nizara ya Nishati kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), UNDP na Ubalozi wa Ireland huku ukibeba kauli mbiu ya 'Kuchagiza Matumizi bora ya Nishati kwa maendeleo endelevu' lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu juu ya mitumizi bora ya Nishati.








 

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI

DED HANANG AKUTANA NA WADAU WA STAKABADHI GHALANI Na, Mudishatv blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay,...

Popular Post