Na. Mohamed CHUMVI, Kiteto
MPAKA sasa idadi ya nguzo za taa barabarani zilizogongwa Kiteto na kuanguka zimefikia tano huku baadhi ya taa hizo zikidaiwa kuwa haziwaki toka zifungwe mapema mwaka huu 2024
Imeelezwa kugongwa kwa taa hizo za barabarani ni kosa, ikizingatiwa kuwa lengo la taa hizo ni kutoa huduma kwa jamii, kwamba ni mpango wa Serikali kupitia TANROAD kuweka taa hizo barabarani kila wilaya na maeneo ya miji inayokuwa.
Diwani wa Kata ya Ndendo jina limehifadhiwa amekumbwa na mkasa wa kugonga taa usiku wa Dec 07. 2024 na kwenda kujisalimisha mwenyewe kituo cha Polisi Kibaya huku vijana walioshuhudia ikigongwa wakiamua kuibeba taa hiyo na kuipeleka Polisi
"Nguzo hii ya ya taa ni ya tano kugongwa na magari na kila inapogongwa haitengenezwi na taa zetu zinaendelea kupungua na hatujui hatma yake na kwa kasi hii kuna uwezekano mkubwa zinaweza kwisha kabisa"amesema Choma Dudu shuhuda
Amesema mbali na taa hizo zilizogongwa kuna taa zingine toka zifungwe na TANROAS hazijawahi kuwaka na kuiomba Swerikali kupitia TANROAD kuja na majibu ya kwanini haziwaki na zilizogongwa na watu kulipa lini huduma itarejezwa
Meneja wa Tarura Kiteto Eng.Edwine Magiri amekuwa mfuatiliaji wa karibu wa taa hizo zinapogongwa, amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa matukio hayo ili sheria ifuate mkondo wake
Imeelezwa kuwa kila anayegonga nguzo ya taa hupewa Contral Number ya kulipa gharama za uharibifu huo jambo ambalo imeelezwa kuwa hakuna mwananchi anayejua namna taa hizo zitakavyorejeshwa


No comments:
Post a Comment