Emmanuel Mwema, DC Kiteto
Na, Mohamed CHUMVI
Baada ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa kukamilika, Serikali wilayani Kiteto imesema itatoa mafunzo kwa wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji ili kuwajengea uwezo.
Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, akizungumza na Mudisha tv amesema, lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi hao ambao baadhi yao ni wapya
"Tunataka kujenga uelewa wa pamoja wa viongozi hao ili wanapotoa huduma wajue msimamo wa Serikali katika kuwatumikia wananchi"amesema Mwema
Amesema maeneo yenye changamoto nyingi za wananchi ni vijijini, huko kuna wenyeviti ambao lazima wapate msimamo wa Serikali na sio vinginevyo
"Migogoro mingi ya wananchi inatoka vijijini, huko ndiko utasikia namna wenyeviti wa vijiji wanavyohusishwa kuuza ardhi na kuacha makovu kwa wananchi"amesema DC Mwema
No comments:
Post a Comment